Mchungaji wa Kanisa
la Free Pentecoste Church of Tanzania (FPCT) Songambele Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma Peter Sungura amefariki dunia katika ajari ya gari liloungua
moto na kuua watu saba na kujeruhi wengine kumi.
Akizungumza
na blog hii, Mchungaji wa Kanisa la FPCT Bigabiro mkoani hapa, David Nkone,
amesema, mchungaji aliyefariki ni Peter Sungura ambaye alikuwa akisimamia
Parishi ya Songambele kwa upande wa kanisa hilo.
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SACP Ferdinand Mtui, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tukio la ajari ya gari kuungua moto na kuua watu saba na kumi kujeruhiwa. |
Amesema,
taarifa za kifo hicho alizipata baada ya kupigiwa simu na mchungaji mwenzake
ambapo alifika hospitali ya Mkoa ya Maweni na alipoingia chumba cha kuhifadhia
maiti alithibitisha kuwa Mchungaji Sungura ni moja ya watu waliofariki katika ajari
hiyo.
“Maelezo
ya Madaktari wanasema katika majeruhi walifikishwa hospitalini hapo na
mchungaji Sungura alikuwemo lakini ilipofika saa 6 usiku alifariki dunia
kutokana na kuungua vibaya” amesema Mch. Nkone.
Aidha
Mch. Nkone amesema, awali kabla ya tukio hilo Mchungaji huyo alikuwepo katika
ofisi za makao makuu ya jimbo (Bigabiro) na baada ya kumaliza masuala ya kikazi
alirudi Kigoma mjini kwa masuala yake binafsi.
“Baada
ya kumaliza shughuri zake huko Mjini ndipo akaanza safari ya kurudi katika
kituo chake cha kazi huko Songambele ambapo ndipo ajari ilimkutia katika gari
alilopanda na kusababisha umauti wake” aliongeza Mch. Nkone
Hata hivyo Mch. Nkone amesema kuwa taratibu za
mazishi zimeshaanza na marehemu atazikwa katika kijiji cha Songambele ambapo
kuna familia yake na maziishi hayo yatafanyika siku ya kesho Desemba 23 mara
baada ya mwili kuwasili kijijini kule.
Kwa
upande wake Mchungaji wa FPCT Mwanga katika Manispaa ya Kigoma-Ujiji, Willison Gwimo, amesema kuwa
taarifa za kifo cha Sungura amezipata mara baada ya kufika hospitalini kwa
lengo la kwenda kuona wagonjwa.
“Baada
ya kufika Hospitali nilikutana na kundi la watu ndipo wakanipa taarifa za ajari
na kuniambia kuwa moja ya watu waliofariki na mchungaji wa kanisa letu yumo,
ikabidi nifike chumba cha kuhifadhia maiti, na kweli nilikuta mwili wa
mchungaji Peter Sungura hivyo nikaamua kuwa taarifu wachungaji wenzangu”
amesema Mch. Gwimo.
Nae Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, SACP
Ferdinand Mtui, amethibitisha kutokea kwa ajari hiyo iliyohusisha gari aina ya Toyota Hiace lenye namba
T.700 kupinduka na kuwaka moto katika Kijiji cha Mwakizega Wilayani Uvinza ikiwa ni majira ya
saa 11 jioni ambapo gari hilo lilikuwa
likitokea Kigoma mjini kuelekea Kijiji cha Subankara.
Alisema kuwa, katika ajari hiyo watu saba
wamefariki dunia na wengine kumi kujeruhiwa na chanzo cha ajari hiyo ni baada
ya dreva kujaribu kuwakwepa watembea kwa mguu waliokuwa wakikatiza barabarani
ambapo gari lilielekea upande mwingine na kugonga ukingo wa barabara na kuangua
kisha kuwaka moto.