Jeshi
la Polisi mkoani Kigoma limewakamata wahamiaji haramu 75 wakijihusisha na
shughuri za kilimo mara baada ya kufanya msako katika Wilaya za Kasulu, Uvinza
na Kigoma mjini.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, SACP
Ferdinand Mtui, amesema kuwa wahamiaji hao walikamatwa wakiwa mashambani
wakiendelea na shughuri za kilimo.
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SACP Ferdinand Mtui, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tukio la kukamatwa kwa wahamiaji haramu. |
Amesema, mbali na kuwakamata wahamiaji hao Polisi waliwakamata pia wahusika wa
mashamba hayo ambao ni Watanzania kutokana na kuvunja sheria kwa kuwatumikisha
raia wa kigeni bila kufuata sheria.
“Wahamaiji
hao watafikishwa mahakamani ili kujibu mashitaka yao ya kuingia nchini kinyume
na sheria wakati wamiliki wa mashamba watatakiwa kujibu mashitaka ya
kuwatumikisha wahamiaji haramu kinyume na sheria” alisema Kamanda Mtui.
Kwa
upande wake Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Kigoma, Maurice Kitinusa, amesem,
taarifa za msako wa wahamiaji haramu anazo ila bado hajapata idadi kamili ya
wahamiaji waliokamatwa.
“Nilipigiwa
simu na Afisa uhamiaji wa Wilaya ya Kasulu kuhusu msako huo na mafanikio yake
ila kwakuwa idadi kamili sijaipata basi tusubiri mpaka baada ya sikukuu ndio
tutatoa idadi kamili kwa mkoa mzima” alisema Kitinusa