Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

May 21, 2018

Taasisi ya Mo Dewji yatoa msaada kwa watoto wenye saratani


Taasisi ya Mo Dewji imetoa msaada kwa watoto wanaopatiwa matibabu ya magonjwa ya saratani katika kituo cha Tumaini la Maisha katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es Salaam.

Msaada ambao umetolewa ni unga wa ngano, khanga na sabuni za kuogea, kufua na kunawia mikono.

Akikabidhi msaada huo, Kaimu Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Belinda Paul alisema taasisi yao itaendelea kuwa na utaratibu wa kutoa msaada katika kituo hicho ili kuwafariji watoto ambao wanapatiwa matibabu.

Alisema hiyo sehemu ya kwanza kutoa msaada kwani wamekuwa na utaratibu wa kusaidia jamii kutokana na uhitaji uliopo hivyo kwa kufanya hivyo wanaamini watakuwa wamegusa maisha ya Watanzania wengi.

Aidha, Paul amewataka watu wengine wenye uwezo kuweka utaratibu wa kusaidia watu wengine wenye uhitaji kama watoto waliopo katika kituo cha Tumaini la Maisha.

Kaimu Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Belinda Paul akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto ambao wanapatiwa matibabu katika kituo cha Tumaini la Maisha.

Kaimu Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Belinda Paul akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasimamizi wa kituo cha Tumaini la Maisha wakati walipokuwa wakikabidhi msaada katika kituo hicho.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (USDM) ambao wanalipiwa gharama za masomo na Taasisi ya Mo Dewji wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wanaopatiwa matibabu katika kituo cha Tumaini la Maisha.

May 7, 2018

RC Makalla awataka wananchi kufanya mazoezi




Taasisi ya Mo Dewji imekuwa miongoni mwa wadhamini ambao kwa kushirikiana na Taasisi ya Tulia Trust wamewezesha kufanyika Tulia Marathon 2018, ikiwa ni mara ya pili kufanya hivyo baada ya mbio za mwaka jana ambazo zilikuwa na mafanikio makubwa.

Akizungumza katika mbio hizo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alisema watu wengi hawana utaratibu wa kufanya mazoezi jambo ambalo sio zuri kiafya na hivyo kuwataka wananchi kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao.

Aidha Makalla alimpongeza Naibu Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwanzilishi wa Taasisi ya Tulia Trust, Dkt. Tulia Ackson kwa kuanzisha mbio hizo ambazo zinasaidia sana mkoa huo kuboresha sekta ya afya na elimu.

“Michezo ni muhimu sana kwa afya zetu … tujifunze na sisi tuanze kufanya mazoezi sababu ni muhimu sana kwa afya zetu. Mimi hapa nilipo sijawahi kuumwa maralia tangu nikiwa kidato cha kwanza lakini sababu nafanya mazoezi. Ukiwa unafanya mazoezi magonjwa haya ya pressure unaachana nayo,” alisema na kuongeza.

“Niseme tunafaidika sana kupitia Trulia Trust kwa mambo ambayo anayafanya, anaupenda mkoa wetu ameboresha miundombinu katika elimu na afya. Alianza kwenye ngoma na sasa anafanya Tulia Marathon na kutokana na marathon hii anakwenda kusaidia afya na elimu.”

Naye Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Rachel Chengula alisema wameamua kushirikiana na Tulia Trust ili kusaidia kuokoa maisha ya Watanzania ambao wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa huduma bora za afya.

“Tunatambua kwamba maisha ya mwanadamu yanaanza mimba inapotungwa hivyo ni muhimu sisi kama sehemu Watanzania tuliojengwa katika misingi ya upendo kuona ni muhimu kushirikiana na serikali na wadau wengine kama Tulia Trust kuweka mazingira bora ya wodi za uzazi ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi nchini,

“Tunapongeza hatua ambazo zinachukuliwa na serikali za kukarabati vituo vya afya katika Halmashauri mbalimbali nchini kwa kujenga na kukarabati majengo ya upasuaji, wodi za wazazi na watoto pamoja na maabara. Tunaamini jitihada hizi zitasaidia kupunguza vifo vya kina mama na watoto nchini,” alisema Chengula.

Awali akizungumza kuhusu Tulia Marathon 2018, Dkt. Tulia alisema fedha ambazo zimepatikana katika mbio za mwaka huu zitatumika kusaidia kuboresha sekta ya elimu na afya kama ilivyokuwa mwaka jana na lengo lao ni kushirikiana na serikali ili kuwezesha wananchi wapate huduma bora za kiafya na elimu bora.

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwanzilishi wa Taasisi ya Tulia Trust, Dkt. Tulia Ackson akiongoza wanariadha waliojitokeza kukimbia katika Tulia Marathon 2018 zilizofanyika Jijini Mbeya.





Naibu Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwanzilishi wa Taasisi ya Tulia Trust, Dkt. Tulia Ackson akielezea mafanikio ambayo Tulia Marathon iliyapata kwa mwaka uliopita na mipango ya mwaka huu.

Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Rachel Chengula akizungumza kuhusu Tulia Marathon 2018 na shughuli ambazo taasisi yao inafanya kwa jamii. Kulia kwake ni Naibu Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwanzilishi wa Taasisi ya Tulia Trust, Dkt. Tulia Ackson.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza namna Tulia Marathon inawasaidia kuboresha sekta ya afya na elimu na kutoa pongezi kwa Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson.


Meneja Miradi wa Taasisi wa Mo Dewji, Rachel Chengula akikabidhi medali na fedha taslimu kwa washindi wa mbio za 5 KM zilizohusisha wanafunzi katika Tulia Marathon 2018 zilizofanyika Jijini Mbeya.






Apr 28, 2018

Woolworths yafungua duka Mlimani City, yajipanga kufunga lingine Dodoma

Mwenyekiti wa Woolworths Tanzania, Ali Mafuruki akikata utepe kuashirikia ufunguzi wa duka duka la nguo la Woolworths lililopo jijini Dar es Salaam. 


Kampuni ya nguo la Woolworths imefungua duka mpya la nguo lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam, likiwa ni duka la tano la kampuni hiyo kwa hapa nchini.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi huo, Mwenyekiti wa Woolworths Tanzania, Ali Mafuruki alisema huo ni mwendelezo kampuni hiyo kufungua maduka ambayo yanauza nguo zenye viwango bora na hivyo kuwataka wananchi kutembelea maduka hayo ili kununua nguo.

Alisema baada ya ufunguzi wa duka hilo wamejipanga kufunga duka lingin makao makuu ya nchi Dodoma ili kuwasogezea bidhaa zao wateja wao na hasa katika kipindi hiki ambacho viongozi wengi wa serikali wamehamia mkoani humo.


"Ni hatua nzuri kwenda mbele, uchumi kwa sasa ni mgumu, wakati wengine wafunga maduka sisi tunafungua kubwa nchini kuliko yote, tumeweza kudhibiti mdororo wa uchumi pamoja na kuwa tumeshindwa kufikia malengo yetu lakini tumekuwa imara,

"Kuanzia mwaka kesho tutaanza kuangalia ujenzi wa duka Dodoma, Dodoma ni makao makuu ya nchi, wapo viongozi wa Serikali na hakuna huduma kama hizi. Tumeanza kuongea na wajenzi ili katika miaka miwili ijayo tufungue duka Dodoma," alisema Mafuruku.

Aidha alizungumza kuhusu wafanyabiasha ambao wanakwepa kodi ambapo kuhusu kampuni yao alisema wamekuwa wakilipa kodi zote ambazo wanatakiwa kulipa na kutumia nafasi hiyo kuwataka wanaokwepa kulipa kodi waache tabia hiyo.


"Mtu anayefanya biashara kwa kutokuwa mwaminfu ipo siku atapambana na serikali, ila sisi sitaki kusikia mfanyakazi anakuja kusema bosi hii pesa nimemhonga mtu wa TRA, sisi kila siku tunawafundisha wafanyakazi wetu walipe kodi zote, hata kama ni kubwa," alisema.

Mwenyekiti wa Woolworths Tanzania, Ali Mafuruki akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa duka la nguo la Woolworths lililopo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Rabi Hume)

Mwenyekiti wa Woolworths Tanzania, Ali Mafuruki  akiingia katika duka la nguo la Woolworths lililopo jijini Dar es Salaam. 





Mar 22, 2018

AJARI YAUA WATU 7 KIGOMA

WATU saba wamefariki dunia baada ya gari  aina ya scania lenye namba za usajili T. 741 AAB baada ya kupinduka katika eneo la mkongoro likitokea kalinzi kuelekea kigoma mjini.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa kigoma Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajari hiyo na kusema kuwa chanzo ni uzembe wa dereva wa gari hilo.

 Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa Maweni Dkt Fadhiri Kibaya majeruhi ni Michael Richard na waliofariki Katika ajari hiyo ni
Deodata Komba, Slimu Hamis, Ramadhani Said,
Elia Katabi,
Nashoni Bilonkwa, Omary Mohamed na  Eliakim Samson.

Mar 21, 2018

MJAMBAZI WAWILI WAUWAWA KIGOMA


Watu  wawili wanaosadikiwa kuwa  majambazi wamefariki dunia huku watatu wakitokomea kusiko julikana baada ya shambulizi baina ya majambazi hao na Askari polisi katika eneo la Makere wilayani Kasulu ambapo katika tukio hilo askari mmoja amejruhiwa mkono.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani hapa  Kamishina Msaidizi Martin Otieno amesema tukio hilo limetokea March 19 lililowahusisha Bukuru Steven ambaye ni mkimbizi na Nobart Andrew  wakiwa wanamiliki silaha mbili  aina ya AK 47 zikiwa na jumla ya  risasi 41.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda Otieno amesema baada ya kuwakamata majambazi hao  walikiri makosa na kwenda na polisi kwa lengo la kuwaonyesha siraha walizoficha sambamba na wenzao
Wakati wakielekea katika poli zilipofichwa siraha hizo ghafla majambazi wengine waliokuwa wamejificha walianza kurusha risasi mfululizo ambazo kwa bahati mbaya ziliwapata majambazi wale wawili waliokuwa na polisi na kufariki dunia huu askali  mmoja akipigwa risasi ya mkono amesema Kamanda Otieno.

Hata hivyo kutokana na kushamiri kwa matukio ya unyanganyi na ujambazi wa kutumia silaha, Kamanda Otieno ametoa siku 30 kwa wakimbizi wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha kwa jeshi la polisi na kuongeza kuwa kutafanyika oparesheni kubwa katika kambi zote za wakimbizi mkoani hapa.

HUMPHREY POLEPOLE APINGWA NA SERIKALI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI

Katibu mwenezi wa CCM Humphrey Polepole 

Manispaa ya Kigoma ujiji imesema itaendelea kusimamia sheria ndogo mpya iliyosainiwa na Ras kupitia TAMISEMI 2017, Sheria ya  kodi ya vibanda shilingi elfu 50 licha ya Jumapili iliyopita Katibu mwenezi wa CCM Humphrey Polepole kueleza kufuta sheria hiyo nakuwatangazia wafanyabiashara wa Kigoma mjini kuendelea na kodi ya zamani  ya elfu 15.

Mstahiki Meya wa Manispaa hii Husen Ruhava ameyasema hayo akiwa ofisini kwake nakwamba anaamini kinachofanywa na kiongozi wa CCM wa ngazi ya juu ni siasa kwasababu maelekzo ya kiserikali hayawezi kupitia kwenye chama.

Msitahiki Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Hussen Ruhava
Meya amewataka watendaji katika ngazi ya manispa wanaohusika na ukusanyaji wa kodi hiyo kutoyumba na badala yake waendelee kukusanya kiasi cha elfu hamsini hadi hapo barua rasmi ya Rais itakapoifika manispaa

Hata Hivyo wanyabiashasha katika manisapaa hii kupitia mwenyekiti wa Jumuia ya wafanyabiashara mkoa, Juma Chaurembo wamefurahishwa na ufutwaji wa kodi hiyo, huku wakisema  watafuta shauri walilofungua mahakamani kuhusu kadhia hiyo.

Jumapili  machi 18 Humphrey Polepole amesema hatua ya kufuta kodi hiyo nikutokana na kuwa kubwa ikipingana na sera ya chama nakwamba ni baada ya kuwasiliana na mamlaka zote za juu za serikali ikiwemo Rais Dk John Pombe Magufuli.